Tuesday, June 10, 2014

YALIYOJIRI VIWANJANI WIKI HII

Kikosi cha Fighters FC wakiwa wanajiandaa na mechi dhidi ya wapinzani wao Alliance FC. Fighters FC waliibuka na ushindi wa goli 5 kwa moja. Goli hizo zilifingwa na Kiduku (1), Hosea (1) na Kadabra (3).
 Kikosi cha Alliance FC kikijiandaa kukabiliana na wapinzani wao Fighters FC. Alliance walilala kwa goli 5 kwa 1
 Baada ya mechi timu zote zilikaa kikao kwa ajili ya kuchagua uongozi mpyaa. na uongozi ulikuwa kama ifuatavyo.
Fighters FC 
Manager ameteuliwa kuwa Amon Nkongoki
Mtunza hazina Sonia Mpinga

Alliance FC
Manager: Tumaini Telespory 
Mtunza hazina: Menlick  Myungile

Daktari wa timu kwa mwaka wa kwanza ameteuliwa Advelina Mpondachuma.


WHITE EAGLES VS BAED 2

Siku ya jumapili kulikuwa na pambano ya kukata na shoka kati ya white eagles vs BAED 2 ambao ulifanyika katika viwanja TTC, matokeo yaliishia goli moja kwa moja. White Eagle walitangulia kufunga mnamo dakika ya tatu (3) lakini BAED 2 walikomboa dakika za majeruhi za kuelekea mapumziko. Kipindi cha pili mwaka wa pili walionekana kucheza kwa ustadi huku safu ya ushambuliaji ya White Eagle ikiwa imepoteana. Moja kati ya wachezaji waling'ara ni pamoja na beki wa White Eagle Sule na Hussen na kwa Mwaka wa pili alikuwa ni Ndondo ambaye alizuia washamuliaji wa White Eagle vilivyo.


KIKOSI CHA BAED 2


VIKOSI VIKIWA VINAJIANDAA KUINGIA UWANJANI 

  Habari imeandaliwa na,

FRANK MSOFE

WAZIRI WA HABARI