Saturday, June 27, 2015

Mashindano ya serikali za mitaa manispaa ya mtwara yapamba moto

Mashindano ya serikali za mitaa manispaa ya mtwara yapamba moto kwa kupatkana kwa timu 4 za kucheza nusu fainal za patkana hapo Jana!!!! Ungana nami hapo baadae kwa taarfa zaid

Monday, March 23, 2015

SIMBA YA STEMMUCO YAIRARUA YANGA

 Klabu ya soka ya Simba ya STEMMUCO, imedhihirisha kuwa siku zote Yanga hafurukuti pindi akutanapo na Simba, baada ya kuinyuka kipigo cha mbwa mwizi, magoli 6-1. Katika mchezo wa kirafiki uliojaa ufundi na burudani ya aina yake, uliyoishuhudia timu ya Yanga ikizabwa magoli hayo mapema kunako sekunde ya 18 kupitia kwa Benjamin a.k.a OKWI, aliyeonekana kuwa mwiba wa timu pinzani, kwani aliweza pia kuipatia Simba magoli katika dakika ya 38 na 64 na kung'ara kama mchezaji bora wa mcezo. Magoli mengine ya Simba yalifungwa na Masoud dakika ya 47, Khamis dakika ya 71 na White dakika ya 85, wakati bao pekee la Yanga likifungwa na Ligwa dakika ya 5. Hadi mwisho wa mchezo huo, Simba ilitoka uwanjani huku ikiwa na utajiri huo wa magoli. 
MASHABIKI WAZALENDO WA STEMMUCO, WALIJITOKEZA PIA KUKITIZAMA KIPUTE HICHO KWANI HAWAKUTAKA KABISA KUSIMULIWA

WACCHEZAJI WA SIMBA, WAKIPONGEZANA BAADA YA KUFUNGA MOJA YA MAGOLI

MCHEZAJI WA SIMBA BENJAMINI, AKISHANGILIA KWA 'KUSLAIDI' KWENYE NYASI ZA UWANJA HUO, HUKU AKIPONGEZWA NA WACHEZAJI WENZAKE BAADA YA KUFUNGA GOLI

WACHEZAJI WA TIMU YA SIMBA WAKIMSIKILIZA KOCHA WAO, LUAMBANO. KABLA YA KUREJEA DIMBANI KWA AJILI YA KIPINDI CHA PILI


KIKOSI CHA TIMU YA SOKA YA YANGA ( STEMMUCO)
BAADHI YA MASHABIKI WA YANGA, WAKIWA NA NYUSO ZA HUZUNI
TIMU YA YANGA IKIWA KATIKA MAPUMZIKO YA KIPINDI CHA KWANZA
MCHEZAJI WA YANGA, KAPAMA WA PILI KULIA, AKIMSHURUTI MWAMUZI, KUMUONESHA KADI YA NJANO BENJAMIN WA KWANZA KULIA, BAADA YA KUVUA FULANA WAKATI AKISHANGILIA GOLI LAKE LA TATU.
HAUKUWA MPAMBANO WA OSEA NA KIDARA PEKEE, HATA NYASI ZA UWANJA WA SHULE YA MSINGI SHANGANI ZILIKUWA KATIKA WAKATI MGUMU.
MASHABIKI WALIOPENDEZA NYUSO, BILA SHAKA HATA MIFEREJI YA NYOYO ZAO, WALIFIKA PIA KUSHUHUDIA PAMBANO HILO LA KUKATA NA SHOKA

                               

                                         " AUNGURUMAPO SIMBA, HUCHEZA NANI?"

                                             IMEANDALIWA NA; ALBINUS GREGORY


Friday, January 23, 2015TANGAZO   TANGAZO  TANGAZO
Ni kwa mara nyingine mashindano ya BIG SCORE yanafikia kilelee siku ya jumamosi baada ya hatua ya makundi kumalizika. Kwenye football leo tar 23/01/2015 siku ya ijumaa kutakuwa na mechi ya nusu fainali kati ya mwaka wa pili B a.k.a Fighter’s FC dhidi ya mwaka wa pili A a.k.a Alliance FC, mechi itachezwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye kiwanja cha jeshini. Mida ya saa 10:00 jioni vijogoo wa mwaka wa tatu watapambana wa mwaka wa kwanza kwenye kiwanja cha jeshini. Fainali itachezwa tar 25/01/2015 kwenye viwanja vya TTC
Netball:
Baada ya mzunguko kumalizika sasa wadada wa mwaka wa pili wanakutana uso kwa uso na wadada wa dip&cet katika mechi ya fainali tar 25/01/2015
Katika viwanja vya TTC . Je wadada wa dip&cet watalipa kisasi kwa kichapo cha mara ya kwanza walichopata kutoka kwa dada zao wa mwaka wa pili? Karibu ujioneee
       Basketball
Baada ya mzunguko sasa mwaka wa pili ambao ndo mabingwa watetezi wataminyana na mwaka wa tatu katika mechi ya fainali itakayofanyika siku ya Jumamosi katika kiwanja cha Bandari Club majira ya saa 10:00 jioni. Je mwaka wa pili wataendeleza ubabe wao wa kutofungwa na madarasa mengine? Karibu ujionee
WOTE MNAKARIBISHWA SANAAAAAA .

Tuesday, June 10, 2014

YALIYOJIRI VIWANJANI WIKI HII

Kikosi cha Fighters FC wakiwa wanajiandaa na mechi dhidi ya wapinzani wao Alliance FC. Fighters FC waliibuka na ushindi wa goli 5 kwa moja. Goli hizo zilifingwa na Kiduku (1), Hosea (1) na Kadabra (3).
 Kikosi cha Alliance FC kikijiandaa kukabiliana na wapinzani wao Fighters FC. Alliance walilala kwa goli 5 kwa 1
 Baada ya mechi timu zote zilikaa kikao kwa ajili ya kuchagua uongozi mpyaa. na uongozi ulikuwa kama ifuatavyo.
Fighters FC 
Manager ameteuliwa kuwa Amon Nkongoki
Mtunza hazina Sonia Mpinga

Alliance FC
Manager: Tumaini Telespory 
Mtunza hazina: Menlick  Myungile

Daktari wa timu kwa mwaka wa kwanza ameteuliwa Advelina Mpondachuma.


WHITE EAGLES VS BAED 2

Siku ya jumapili kulikuwa na pambano ya kukata na shoka kati ya white eagles vs BAED 2 ambao ulifanyika katika viwanja TTC, matokeo yaliishia goli moja kwa moja. White Eagle walitangulia kufunga mnamo dakika ya tatu (3) lakini BAED 2 walikomboa dakika za majeruhi za kuelekea mapumziko. Kipindi cha pili mwaka wa pili walionekana kucheza kwa ustadi huku safu ya ushambuliaji ya White Eagle ikiwa imepoteana. Moja kati ya wachezaji waling'ara ni pamoja na beki wa White Eagle Sule na Hussen na kwa Mwaka wa pili alikuwa ni Ndondo ambaye alizuia washamuliaji wa White Eagle vilivyo.


KIKOSI CHA BAED 2


VIKOSI VIKIWA VINAJIANDAA KUINGIA UWANJANI 

  Habari imeandaliwa na,

FRANK MSOFE

WAZIRI WA HABARI

 

 

 


Wednesday, December 11, 2013

PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI YA MAHAFALI YA MWAKA WA TATU TAR 6/12/2013

Serikali ya Wanachuo (STEMMUCSO) inawapongeza wanachuo wenzetu wote waliofanikiwa kumaliza salama na hatimaye leo wmetunukiwa shahada zao na tunawaombea heri na baraka huko muendako muweze kufanikiwa zaidi katika maisha yenu


Askofu Gabriel akiwaongoza maaskofu wengine,mapadre wakufunzi wahitimu na waumini kutoka kanisani mara baada ya kumalizika kwa misa ya mahafali

Picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa ibada ya misa ya mahafali


                                      Wanakwaya wakiongoza maandamano ya kutoka kanisani
Maaskofu,Mapadre,wakufunzi na wahitimu wa mwaka wa tatu wakiwa katika picha ya pamoja

Waziri wa jinsia wa serikali ya wanachuo Mh Happy akigawa vitabu vya mahafali kwa wahitimu

Rais wa serikali ya wanachuo Mh Mwatebela Agrey kushoto akiwa na Mh Patrick Patrick ambaye ni waziri ofisi ya rais kabla ya kuanza rasmi kwa sherehe  ya mahafali

Wakufunzi wakiwa katika maandamano kuelekea jukwaa kuu tayari kwa kuanza sherehe ya mahafali

Mkuu wa chuo akiwaongoza mgeni rasmi na wageni wengine waalikwa katika Jukwaa kuu 

Wahitimu wa shahada ya sanaa na ualimu wakiwa katika jukwaa

wahitumu wa shahada ya elimu na sanaa wakisubiri kutunukiwa shahada zao

Mkuu wa chuo Father Dr. Longino akitoa nasaha zake kwa wahitimu


Wahitimu wa shahada ya Mahusiano ya jamii(Sociology)wakifurahia mara baada ya kutunukiwa shahada zao

Wahitimu wakipongezana
Mgeni rasmi akitoa nasaha zake kwa wahitimuMmoja wa wahitimu akishangilia mara baada ya kutunukiwa shahada


Wanakamati ya ulizi walikua mstari wa mbele kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.

Wahitimu wa shahada ya elimu na sanaa

Naibu waziri wa habari wa serikali iliyopita Mh Francis Mtunda a.k.a Jasiri kulia akiwa katika picha ya pamoja na Naibu waziri wa habari wa sasa Mh Danstan Mahiza mwenye shti jeupe

Picha ya pamoja ya Maaskofu,Mgeni rasmi,Mkuu wa chuo na wakufunzi mara baada ya kumalizika kwa sherehe za mhafali

Father Champlain akifungua sherehe za mahafali kwa sala

Katibu wa wizara ya habari Mh Nassor kushoto akiwa na wanakamati ya ulinzi

Mwishowe wanakamati  walijumuika pamoja na kuburudikaPicha zote na 
Danstan Mahiza
Naibu waziri wa habari
STEMMUCSO


Saturday, November 9, 2013

SPECIAL ANNOUNCEMENT TO ALL EXPECTED GRADUANDS OF STEMMUCO (2013)

Preliminary list for expected graduands who will attend the 2nd University Graduation ceremony on 5th December 2013 will be released on 5th November 2013.

NOTE: Students with academic problems will have to
submit their complaints to the Examinations Officer from 5th to 7th November 2013 (either physically or through e
mail).
E Mail Address: sr.flora71@yahoo.com
Tel: 0787 -141722


Thursday, November 7, 2013

TEACHING POLICY

DOWNLOAD TEACHING POLICY HAPAhttps://drive.google.com/file/d/0B6XZvPZWiHcoVkNtOS15Nm

WELCOME FIRST YEAR EVENT

Serikali ya wanachuo STEMMUCSO  kupitia kwa wizara yake ya Maafa na  Starehe inapenda kuwafahamisha kuwa siku ya Ijumaa tar 08/11/2013 kuanzia saa moja usiku kutakua na bash/party ya kuwakaribisha wanafunzi wa mwaka wa kwanza(certificate,Diploma na Shahada) itakayofanyika katika ukumbi wa Makonde Beach Club.


Hakutakua na kiingilio kwa wanachuo wote wa STEMMUCO,ila kwa wale ambao watapenda kuungana nasi watalipa kiingilio cha Tsh 3000/= tu.
Unakumbushwa kufika na kitambulisho chako cha chuo.


                                    Wote mnakaribishwa!


                                                                    Danstan Mahiza
                                                              Naibu Waziri wa Habari
                                                                     STEMMUCSO

Friday, November 1, 2013

KIKAO CHA VIONGOZI MBALIMBALI WA WANACHUO NA WAJUMBE/VIONGOZI KUTOKA TCU

Kikao hicho kiliwakutanisha wajumbe/viongozi kutoka Tanzania Commission for Universities (TCU) uongozi wote wa STEMMUSO ,Rais,Makamu wa Raisi,waziri mkuu,baraza lote la mawaziri na makatibu.Pia walikuwepo Wabunge wa Stemmusco na MaCR wa facult zote na wa kila somo.

Lengo kuu la kikao hicho lilikua ni kujadili changamoto mbalimbali zinazo kikabili chuo chetu.Wawakilishi hao wa wanachuo waliweza kuwasilisha changamoto nyingi pamoja na mazuri mengi tu ambayo yamefanyika chuoni kwetu pia walijaribu kutoa ushauri wa nini kifanyike katika kukiboresha chuo chetu na kuwafanya wanachuo wote wayafurahie maisha ya chuo pamoja na kuzingatia ubora  unaotakiwa kwa sheria za vyuo vikuu vyote nchini unafikiwa....

Viongozi wa Stemmusco wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe kutoka TCU akiwemo Dr,Kitila Mkumbo(mwenye miwani katikati)Mara baada ya kumalizika kwa kikao katika ukumbi wa Main Hall

Wawakilishi wa wanachuo wakiwa makini kusikiliza nini kinaelezwa katika kikao hicho na viongozi kutoka TCU

Dr. Kitila Mkumbo Akijitambulisha kwa viongozi mbalimbali wa wanachuo 

Rais wa Stemmusco Mh.Agrey Mwatebela nae ilipata nafasi ya kuzungumza machche katika kikao hicho                                                       
                                                     
                                                              Danstan Mahiza
                                                        Naibu Waziri wa Habari
                                                             STEMMUCSO