Saturday, September 8, 2012

YAH: HOSTELI ZA CHUO.

Hii ni kuutaarifu Umma wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara kwamba Hosteli za Chuo katika mwaka wa masomo 2012/2013 ni kwa ajili ya Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza tuu na wale wanafunzi wenye Mahitaji maalumu. Hivyo basi wale walioshikilia vyumba kwa kuvifunga na kuondoka na funguo za vyumba husika wanapaswa kurudisha mara moja kwa Kiongozi Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Udahili, Ukaribisho, na Makazi kwa namna yeyote ile na kwa haraka itakavyowezekana. Wale wanafunzi wenye mahitaji maalum watume barua za maombi ya kuishi hosteli kwenda kwa Mwadili wa Wanafunzi STEMMUCO. Barua zitumwe kwenye anuani ya barua pepe ifuatayo superintendent.stemmuso@gmail.com Mwisho wa kupokea maombi hayo ni Septemba 16, 2012. Upatapo tangazo hili umuarifu na mwenzako.

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais.
STEMMUCO.

Friday, September 7, 2012

ATTENTION TO ALL FIRST YEAR STUDENTS

Those who have been selected to join the various programmes in our University College and they would wish to have admission letters for permissions from their job stations and/or scholarship/sponsorship  purposes, you may send your inquiry to The Admissions Officer (Mr. Buteta) through the following numbers ; +255 (0) 655- 467-694, +255 (0) 767-467-694, +255 (0) 783 - 467-694 or by using the following e-mail addresses; buteta@yahoo.co.uk, buteta@stemmuco.ac.tz, admissions@stemmuco.ac.tz.

Karibu Sana!

SALLA, Donati P.
The STEMMUSO Vice President.

Re: THE OPENING DATES AT STELLA MARIS MTWARA UNIVERSITY COLLEGE.

This is to inform you Officially that, The following are the dates of opening the 2012/2013 Academic year in Our College:
1) All First year Students ( Certificates, Bachelor degrees, and Master  Students) they shall commence the 2012/2013 Academic year on Monday September 17, 2012.

2) The Continuing Students BASO2, & BASO3 Shall commence the 2012/2013 Academic year on Monday September 24, 2012.

3) The Continuing Students (BAED2, BAED3, BAPHILED2, BAPHILED3) Shall commence the 2012/2013 Academic year on Wednesday October 24, 2012.

SALLA, Donati P.
The STEMMUSO Vice President.

Thursday, September 6, 2012

YAH: UTEUZI WA NDG. NG'HUMBUBANHU, Abel NA KUTUNUKIWA HATI YA UWAJIBIKAJI KATIKA SERIKALI KWA NDG: FRANCIS CLEMENT

Hii ni kuutaarifu Umma wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara kwamba, Mhe. Rais KAMILI, John C. wa Serikali ya Wanafunzi STEMMUSO amemteua Ndg. NG'HUMBUBANHU, Abel kuwa Kiongozi mwandamizi Ofisi ya Rais, kwa ajili ya kushughulikia Masuala ya udahili wa wanafunzi hapa Chuoni. Pia katika Shughuli zake za leo Mhe.Rais amemtunuku Ndg. Clement Francis hati ya Uwajibikaji katika Serikali, pamoja na kumteua rarsmi kama Msimamizi Mwandamizi wa Ustawi wa Wanafunzi na Chuo, katika Serikali ya Wanafunzi - STEMMUSO. Pamoja na hayo Mhe.Clement ataendelea kuwa Naibu Waziri wa Habari na Masuala ya Chuo huku akifanya kazi ya Usimamizi Mwandamizi katika ofisi ya Waziri Mkuu - STEMMUSO.
Mwisho Mhe.Rais amewapongeza viongozi hawa na kuwatakia kila kheri katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Aluta Continua" Tuongeze jitihada katika kulijenga jiji la Mungu!

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais
CHUO KIKUU CHA STELLA MARIS MTWARA.




YAH: MALIPO YA POSHO YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA MWAKA WA TATU KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012

Hii ni kuwataarifu wanafunzi wote waliomaliza mwaka wa tatu Chuoni STEMMUCO katika mwaka wa masomo 2011/2012 kwamba, malipo ya posho ya kufanya utafiti ni shilingi 100,000/= TZS (Laki moja tu ya Kitanzania). Pia kwa mujibu wa kanuni za utoaji wa fedha za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, ni kwamba haturuhusiwi kufanya malipo yoyote kwa Mwanafunzi ambaye hajasaini taarifa za uthibitisho wa kupokea malipo hayo. Hivyo basi wale wanachuo walimaliza masomo yao katika mwaka tajwa hapo juu, kama wapo jirani na Chuo wanashauriwa kufika hapa chuoni na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Mwadili wa wanafunzi kwa ajili ya kusaini malipo yao. Wale wanachuo ambao wapo mbali mnashauriwa kuwa watulivu hadi siku ya mahafali (ambapo ni mwezi Desemba) hivyo basi utakapokuja Chuoni kwa ajili ya Mahafali ndipo hapo utakaposaini na kulipwa malipo yako. Kama unaona kwamba unaweza kuja hapa chuoni na kusaini malipo yako basi hakuna kizuizi chochote kwani unaweza kuja ukasaini, kisha ukapewa malipo yako.

Ofisi ya Mwadili wa Wanafunzi pamoja Ofisi ya Waziri wa Mikopo - STEMMUSO, Kwa pamoja tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais
CHUO KIKUU CHA STELLA MARIS MTWARA.

Wednesday, September 5, 2012

HABARI MPASUKO (Breaking News)

Hii ni kuwataarifu Wanafunzi wote wa Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara ambao wanatarajia kuingia Mwaka wa pili na wa tatu katika mwaka wa masomo 2012/2013 na pia ni wafaidika wa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu - Tanzania  kwamba, leo Jumatano tarehe 05 Septemba 2012, fedha za posho kwa ajili ya Mafunzo kwa vitendo zimekwisha wekwa katika akaunti zenu. wale wenye matatizo mbalimbali yanahusu mikopo wanaweza kutuma taarifa za matatizo yao kupitia mikopo.stemmuso@gmail.com ili matatizo yao yaweze kutatuliwa. Kwa wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaombwa kuwa na uvumilivu kidogo wakati Afisa Mikopo wa Chuo akiendelea kuandaa taratibu za kisheria kwa ajili ya Malipo yao.

Nawatakieni siku njema.

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais
STELLA MARIS MTWARA UNIVERSITY COLLEGE.

YAH: TANZIA YA KIFO CHA DEZDER DENICE

Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi STEMMUSO unasikitika kuwataarifu juu ya kifo cha mwanafunzi mwenzetu aliyekuwa mwaka wa pili na kutaraji kuingia mwaka wa tatu 2012/2013 ambaye Jina lake ni DEZDER, Denice au kwa jina maarufu "Kaboy" kwamba amefariki usiku wa kuamkia Jumatatu tarehe 03 September 2012. Marehemu amezikwa kijijini kwao Rubya, Mkoani Kagera katika siku ya Jumanne tarehe 04 September 2012. Kwa upande wa Chuo, Chuo Kiliwakilishwa na Padre kutoka SAUT Main Campus na kwa upande wa serikali ya Wanafunzi, Tuliongozwa na Mhe: Deusdedith Mathius - Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi STEMMUSO. Chuo kilitoa rambirambi ya fedha taslimu kwenye familia ya marehemu na pia  baadhi ya wanafunzi wenzetu wa STEMMUCO waishio mkoani Kagera walihudhuria maziko hayo.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa! Jina la Bwana libarikiwe na Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi Amen.

SALLA, Donati P.
Makamu wa  Rais
STELLA MARIS MTWARA UNIVERSITY COLLEGE.

Monday, September 3, 2012

RE:PHILOSOPHY OF EDUCATION (EF:112)

This is to inform all students who expect to seat for the Philosophy of Education (EF:112) as their Special/Supplementary Examination that, the aforesaid examination (EF:112) shall be done by tommorow Tuesday 04th September 2012 at MTR 7 From 16:00 Hrs to 19:00 Hrs. If you have got this information please may you inform your colleague.

SALLA, Donati P.
The STEMMUSO Vice President.

Sunday, September 2, 2012

YAH: MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STEMMUCO

Hii ni kuutaarifu Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba, Majina ya watu waliochaguliwa kujinga na Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara katika programu mbalimbali yametangazwa jana rasmi na Afisa Udahili wa Chuo kupitia wavuti yetu ya www.stemmuco.ac.tz. Pia fomu za kujiunga na Chuo (Joining Instructions) zinapatikana katika wavuti hiyo ya www.stemmuco.ac.tz ikiwa ni pamoja na mchanganuo wa malipo ya ada. Kama wewe ni mmoja kati ya waliochaguliwa kujiunga na STEMMUCO, unapaswa kupakua (download) fomu inayokuhusu na kuijaza kwa umakini kisha kuja nayo hapa chuoni. Majina ya Wanafunzi waliochaguliwa katika Chuo Chetu ni wote kuanzia wale wa MBA (Master of Business Administration), Shahada ya Kwanza (Degree programmes), na Cheti katika fani mbalimbali.

SALLA, Donati P.
MAKAMU WA RAIS
STELLA MARIS MTWARA UNIVERSITY COLLEGE
 

RE: THE RELEASE OF 02ND SEMISTER RESULT OF THE YEAR 2011/2012 FOR THIRD YEAR STUDENTS.

The examination results of the second semester in 2011/2012 Academic Year have been released for third year students ONLY. These results include the results for students who are indebted by the college and those who have completed the payments of the tuition fees and all other required financial contributions. Recently the results are posted on the College noticeboard which is found in Dispensary area. You are advised to look for your relative and/or a friend who is present around the college, so that he/she may go and look for your results. Keep in mind that the supplementary and special examinations will be done starting from tomorrow Monday 03rd September 2012 up to Saturday 08th September 2012.

SALLA, Donati P.
The Vice President
Stella Maris Mtwara University College.

Saturday, August 18, 2012

YAH: TAREHE ZA KWENDA TP.

Hii ni kuwafahamisha wanafunzi wote wa BAED1 & BAED2 Kwamba Mazoezi ya Ualimu
 (Teaching practicals) yataanza tarehe 10/09/2012 - 20/10/2012. Unakumbushwa kuwahi mapema kwenye kituo chako cha mazoezi na kujiandaa mapema kwa ajili ya kufanyiwa tathmini (Assesssment) na wahadhiri kutoka chuoni kwetu STEMMUCO.

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais.
STEMMUCO.

Friday, August 17, 2012

RE: SUPPLEMENATY AND SPECIAL EXAMINATIONS

This is to inform all students who are needed to seat for supplementary Examinations and Special examinations that, the aforesaid examinations shall be seated by 03rd - 08th September 2012 and not Otherwise!
NB: If you will happen to miss any examination without information and/or undue factor for the miss of exam, you will cease to exist from studies.
SALLA, Donati P.
The Vice President.
STEMMUSO.

TAARIFA JUU FEDHA ZA UTAFITI, TP, PT,NA MATATIZO YA MITIHANI.

Hii ni kuwataarifu wanafunzi wote wanaohusika na masuala tajwa hapo juu kwamba Fedha za Utafiti, PT, na TP, Zinatarajiwa kutoka kwanzia wiki ya tarehe 22/08/2012 pia matatizo yote ya Mitihani yatatuliwa kuanzia wiki hiyo ya 22/08/2012 Na Mhe. Francis Clement - Naibu Waziri wa Habari na Masuala ya Chuo. Unaweza Kuwasiliana na Mhe. Naibu Waziri kwa namba 0717 521230.
Ofisi ya Rais inawaomba radhi kwa usumbufu wowote ambao utajitokeza.
Imetolewa na;-
Ndg: SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais.
STEMMUSO.

Saturday, July 21, 2012

TAARIFA RASMI KWA UMMA WA WANAFUNZI STEMMUCO

YAH: MALIPO YA FEDHA ZA MAZOEZI KWA VITENDO, TAREHE YA KUFANYA

          MITIHANI YA KUJAZILIA (SUPPLEMENTARY & SPECIAL EXAMINATIONS), 

          MALIPO YA FEDHA ZA UTAFITI KWA MWAKA WA TATU WALIOMALIZA 

          MASOMO YAO KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012, PAMOJA NA 

          TARATIBU ZA MAOMBI YA KOZI NA PROGRAMU MBALIMBALI KATIKA

          CHUO CHETU CHA STELLA MARIS MTWARA.

 Baada ya Kupokea simu na meseji mbalimbali zinazotaka ufafanuzi juu ya masuala tajwa hapo juu, kwa niaba ya Wizara ya Mikopo, Wizara ya Habari na Masuala ya Chuo, pamoja na Wizara ya Elimu, ninatoa taarifa rasmi ya masuala tajwa hapo juu kama ifuatavyo;
(1) MALIPO YA FEDHA ZA MAZOEZI KWA VITENDO.
Mheshimiwa Rais aliniagiza mnamo tarehe 16/07/2012 kufika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ili Serikali ya STEMMUSO, kwa niaba ya wanafunzi, iweze kupata muafaka au hatma ya malipo ya fedha za mazoezi kwa vitendo zinazofahamika kama "Boom la field" Nilikwenda tarehe 17/07/2012 kuhakiki taarifa hizo. Baada ya kufika bodi nilikuta nyaraka za ulipwaji wa fedha, pamoja na hundi ya fedha iliyokuwa imekwisha andikwa kwa ajili ya malipo ya wanafunzi wa STEMMUCO ambapo hundi hiyo pamoja na oradha ya majina ya walipwaji wa fedha hizo ilikuwa imekwisha andaliwa na Waziri wa Mikopo wa STEMMUSO kwa kushirikiana na Mwadili/Mshauri wa Wanafunzi. Niliwauliza Bodi ya Mikopo Kulikoni? Mbona kuna makaratasi lakini hakuna fedha?Bodi ya Mikopo hawakuwa na majibu yanayoeleweka ila walisema kuwa kuanzia tarehe 17/07/2012 hadi Katikati ya Mwezi wa Augusti Ndani ya kipindi hicho katika muda wowote ule Fedha za field zitaingizwa kwenye akaunti zetu. Jambo lililoonyesha wazi kabisa kwamba Bodi ya Mikopo kwa sasa hawana fedha. Hivyo basi naomba nichukue nafasi hii kuomba wanafunzi na kuwasihi kwa dhati kwamba tuwe watu wenye subira na wavumilivu katika kipindi chote hiki ambacho ni kigumu. Serikali yenu mliyoipa dhamana itahakikisha kwamba inashughulikia suala hili kwa haraka, na kwa umakini mkubwa katika muda mwafaka.

(2) TAREHE YA KUFANYA MITIHANI MAALUM NA ILE YA KUJAZILIA (Supplementary &Special Examinations)
Tarehe iliyokuwa imetangazwa awali ni tarehe 03/09/2012 - 08/09/2012. Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kubadilika kwa tarehe hizo ila baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Mitahani ya semista ya pili Mnamo mwezi August, tutatoa taarifa mpya juu ya kubakia kwa tarehe tajwa kwa ajili ya ufanyaji wa mitihani hiyo, au mabadiliko ya tarehe nyingine kwa ajili ya kufanya mitahani husika.
(3) FEDHA ZA MALIPO YA UTAFITI KWA AJILI YA MWAKA WA TATU WALIOMALIZA.
Fedha hizo zipo kwa kuwa ni moja kati ya masuala niliyoyashughulikia nilipokwenda bodi ya Mikopo ila zitatoka wakati wa malipo ya fedha za mazoezi ya Vitendo kwa mwaka wa kwanza na wa pili. Kwa maelezo zaidi soma tangazo namba moja hapo juu.
(4) MAOMBI YA KUSOMA KOZI MBALIMBALI HAPA CHUONI. 
Maelekezo yote ya uombaji wa kozi na programu mbalimbali hapa chuoni pamoja na taratibu na sifa za uombaji, pamoja na makataa (Deadline) ya uombaji wa kozi na programu zote yanapatikana katika tovuti ya chuo ambayo ni Http://www.stemmuco.ac.tz Hivyo basi serikali ya STEMMUSO inawashauri wadau wake kufungua wavuti ya chuo ili kupata taarifa hizo. Pia wanafunzi waliomaliza mwaka wa tatu mnamo mwaka 2011/2012 wanaruhusiwa kuomba programu ya MBA (Master of Business Administration) ilimradi tu wawe na sifa stahiki.



SALLA, Donati P.
MAKAMU WA RAIS
STEMMUSO

Wednesday, July 4, 2012

NAFASI ZA KAZI (VACANCIES)

Hii ni kuwataarifu wanafunzi wote wa Stella Maris Mtwara University College waliohitimu masomo yao ya shahada ya Kwanza kwamba, Kuna nafasi za kazi ya Uhadhiri Msaidizi (Tutorial Assisatants) katika kozi mbalimbali zinazofundishwa hapa chuoni. Kwa maelezo zaidi fungua wavuti ya chuo ambayo ni Http://www.stemmuco.ac.tz kisha fungua sehemu iliyoandikwa "News" utapata taarifa zote kuhusu nafasi hizi za ajira hapa chuoni.
Kwa taarifa juu ya tarehe rasmi ya kufanya mitihani ya kujazilia yaani "Supplementary Examinations" tutawapa taarifa rasmi hapo baadae.
SALLA, Donati P.
MAKAMU WA RAIS
STEMMUCO