Wednesday, September 5, 2012

HABARI MPASUKO (Breaking News)

Hii ni kuwataarifu Wanafunzi wote wa Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara ambao wanatarajia kuingia Mwaka wa pili na wa tatu katika mwaka wa masomo 2012/2013 na pia ni wafaidika wa mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu - Tanzania  kwamba, leo Jumatano tarehe 05 Septemba 2012, fedha za posho kwa ajili ya Mafunzo kwa vitendo zimekwisha wekwa katika akaunti zenu. wale wenye matatizo mbalimbali yanahusu mikopo wanaweza kutuma taarifa za matatizo yao kupitia mikopo.stemmuso@gmail.com ili matatizo yao yaweze kutatuliwa. Kwa wanafunzi wa mwaka wa tatu wanaombwa kuwa na uvumilivu kidogo wakati Afisa Mikopo wa Chuo akiendelea kuandaa taratibu za kisheria kwa ajili ya Malipo yao.

Nawatakieni siku njema.

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais
STELLA MARIS MTWARA UNIVERSITY COLLEGE.

No comments: