Saturday, September 8, 2012

YAH: KUTOLEWA KWA TAARIFA RASMI NA YA MWISHO KUHUSU MPANGILIO WA VITUO VYA KUFANYIA MAZOEZI YA UALIMU (TP ALLOCATIONS)


Hii ni kuwataarifu wanafunzi wote wa Mwaka wa Kwanza ambao wanatarajia kuingia Mwaka wa Pili, na wale wa Mwaka wa pili wanaotarajia kuingia Mwaka wa tatu katika Mwaka wa Masomo 2012/2013 katika  Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara kwamba, taarifa rasmi ya matokeo ya kupangwa kwenye vituo vya kufanyia mazoezi ya Ualimu (Teaching Practices) inapatikana katika wavuti ya Http://www.stemmuco.ac.tz hivyo basi unapaswa kufungua wavuti tajwa ili ufahamu ni wapi ulipopangwa kufanya Mazoezi ya Ualimu.
NB: (1)Hapatakuwepo na mabadiliko yoyote ya Kituo hivyo basi NENDA KWENYE KITUO ULICHOPANGIWA MOJA KWA MOJA. Pia hupaswi kuchelewa kwenye Kituo kwa sababu kama Mtathmini atapita katika kituo chako na akakukosa  utapaswa kurudia mwaka wa masomo kwani TP ni sehemu ya mtihani wa kitaaluma hapa Chuoni.
(2) Kwa tatizo lolote litakalo jitokeza wakati ukiwa kwenye mazoezi  unapaswa kuwasiliana na Mratibu wa eneo lako au kupiga namba za simu zifuatazo 0713 286 999, 0717 521230
, 0765 194 201. 
(3) Baada ya kumaliza Mazoezi unapaswa kuja Chuoni Moja kwa Moja kwa ajili ya Masomo kama ratiba inavyoelekeza. (Kwa Maelezo kuhusu tarehe za kufungua Chuo pekua katika Masjala ya wazi ya blogu hii).

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais.
CHUO KIKUU CHA STELLA MARIS MTWARA.

No comments: