Friday, January 23, 2015TANGAZO   TANGAZO  TANGAZO
Ni kwa mara nyingine mashindano ya BIG SCORE yanafikia kilelee siku ya jumamosi baada ya hatua ya makundi kumalizika. Kwenye football leo tar 23/01/2015 siku ya ijumaa kutakuwa na mechi ya nusu fainali kati ya mwaka wa pili B a.k.a Fighter’s FC dhidi ya mwaka wa pili A a.k.a Alliance FC, mechi itachezwa majira ya saa 8:00 mchana kwenye kiwanja cha jeshini. Mida ya saa 10:00 jioni vijogoo wa mwaka wa tatu watapambana wa mwaka wa kwanza kwenye kiwanja cha jeshini. Fainali itachezwa tar 25/01/2015 kwenye viwanja vya TTC
Netball:
Baada ya mzunguko kumalizika sasa wadada wa mwaka wa pili wanakutana uso kwa uso na wadada wa dip&cet katika mechi ya fainali tar 25/01/2015
Katika viwanja vya TTC . Je wadada wa dip&cet watalipa kisasi kwa kichapo cha mara ya kwanza walichopata kutoka kwa dada zao wa mwaka wa pili? Karibu ujioneee
       Basketball
Baada ya mzunguko sasa mwaka wa pili ambao ndo mabingwa watetezi wataminyana na mwaka wa tatu katika mechi ya fainali itakayofanyika siku ya Jumamosi katika kiwanja cha Bandari Club majira ya saa 10:00 jioni. Je mwaka wa pili wataendeleza ubabe wao wa kutofungwa na madarasa mengine? Karibu ujionee
WOTE MNAKARIBISHWA SANAAAAAA .

No comments: