Monday, March 23, 2015

SIMBA YA STEMMUCO YAIRARUA YANGA

 Klabu ya soka ya Simba ya STEMMUCO, imedhihirisha kuwa siku zote Yanga hafurukuti pindi akutanapo na Simba, baada ya kuinyuka kipigo cha mbwa mwizi, magoli 6-1. Katika mchezo wa kirafiki uliojaa ufundi na burudani ya aina yake, uliyoishuhudia timu ya Yanga ikizabwa magoli hayo mapema kunako sekunde ya 18 kupitia kwa Benjamin a.k.a OKWI, aliyeonekana kuwa mwiba wa timu pinzani, kwani aliweza pia kuipatia Simba magoli katika dakika ya 38 na 64 na kung'ara kama mchezaji bora wa mcezo. Magoli mengine ya Simba yalifungwa na Masoud dakika ya 47, Khamis dakika ya 71 na White dakika ya 85, wakati bao pekee la Yanga likifungwa na Ligwa dakika ya 5. Hadi mwisho wa mchezo huo, Simba ilitoka uwanjani huku ikiwa na utajiri huo wa magoli. 
MASHABIKI WAZALENDO WA STEMMUCO, WALIJITOKEZA PIA KUKITIZAMA KIPUTE HICHO KWANI HAWAKUTAKA KABISA KUSIMULIWA

WACCHEZAJI WA SIMBA, WAKIPONGEZANA BAADA YA KUFUNGA MOJA YA MAGOLI

MCHEZAJI WA SIMBA BENJAMINI, AKISHANGILIA KWA 'KUSLAIDI' KWENYE NYASI ZA UWANJA HUO, HUKU AKIPONGEZWA NA WACHEZAJI WENZAKE BAADA YA KUFUNGA GOLI

WACHEZAJI WA TIMU YA SIMBA WAKIMSIKILIZA KOCHA WAO, LUAMBANO. KABLA YA KUREJEA DIMBANI KWA AJILI YA KIPINDI CHA PILI


KIKOSI CHA TIMU YA SOKA YA YANGA ( STEMMUCO)
BAADHI YA MASHABIKI WA YANGA, WAKIWA NA NYUSO ZA HUZUNI
TIMU YA YANGA IKIWA KATIKA MAPUMZIKO YA KIPINDI CHA KWANZA
MCHEZAJI WA YANGA, KAPAMA WA PILI KULIA, AKIMSHURUTI MWAMUZI, KUMUONESHA KADI YA NJANO BENJAMIN WA KWANZA KULIA, BAADA YA KUVUA FULANA WAKATI AKISHANGILIA GOLI LAKE LA TATU.
HAUKUWA MPAMBANO WA OSEA NA KIDARA PEKEE, HATA NYASI ZA UWANJA WA SHULE YA MSINGI SHANGANI ZILIKUWA KATIKA WAKATI MGUMU.
MASHABIKI WALIOPENDEZA NYUSO, BILA SHAKA HATA MIFEREJI YA NYOYO ZAO, WALIFIKA PIA KUSHUHUDIA PAMBANO HILO LA KUKATA NA SHOKA

                               

                                         " AUNGURUMAPO SIMBA, HUCHEZA NANI?"

                                             IMEANDALIWA NA; ALBINUS GREGORY


No comments: