Thursday, September 6, 2012

YAH: MALIPO YA POSHO YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WALIOMALIZA MWAKA WA TATU KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012

Hii ni kuwataarifu wanafunzi wote waliomaliza mwaka wa tatu Chuoni STEMMUCO katika mwaka wa masomo 2011/2012 kwamba, malipo ya posho ya kufanya utafiti ni shilingi 100,000/= TZS (Laki moja tu ya Kitanzania). Pia kwa mujibu wa kanuni za utoaji wa fedha za Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu, ni kwamba haturuhusiwi kufanya malipo yoyote kwa Mwanafunzi ambaye hajasaini taarifa za uthibitisho wa kupokea malipo hayo. Hivyo basi wale wanachuo walimaliza masomo yao katika mwaka tajwa hapo juu, kama wapo jirani na Chuo wanashauriwa kufika hapa chuoni na kwenda moja kwa moja kwenye ofisi ya Mwadili wa wanafunzi kwa ajili ya kusaini malipo yao. Wale wanachuo ambao wapo mbali mnashauriwa kuwa watulivu hadi siku ya mahafali (ambapo ni mwezi Desemba) hivyo basi utakapokuja Chuoni kwa ajili ya Mahafali ndipo hapo utakaposaini na kulipwa malipo yako. Kama unaona kwamba unaweza kuja hapa chuoni na kusaini malipo yako basi hakuna kizuizi chochote kwani unaweza kuja ukasaini, kisha ukapewa malipo yako.

Ofisi ya Mwadili wa Wanafunzi pamoja Ofisi ya Waziri wa Mikopo - STEMMUSO, Kwa pamoja tunaomba radhi kwa usumbufu uliojitokeza.

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais
CHUO KIKUU CHA STELLA MARIS MTWARA.

No comments: