Saturday, September 8, 2012

YAH: HOSTELI ZA CHUO.

Hii ni kuutaarifu Umma wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara kwamba Hosteli za Chuo katika mwaka wa masomo 2012/2013 ni kwa ajili ya Wanafunzi wa Mwaka wa Kwanza tuu na wale wanafunzi wenye Mahitaji maalumu. Hivyo basi wale walioshikilia vyumba kwa kuvifunga na kuondoka na funguo za vyumba husika wanapaswa kurudisha mara moja kwa Kiongozi Mwandamizi anayeshughulikia Masuala ya Udahili, Ukaribisho, na Makazi kwa namna yeyote ile na kwa haraka itakavyowezekana. Wale wanafunzi wenye mahitaji maalum watume barua za maombi ya kuishi hosteli kwenda kwa Mwadili wa Wanafunzi STEMMUCO. Barua zitumwe kwenye anuani ya barua pepe ifuatayo superintendent.stemmuso@gmail.com Mwisho wa kupokea maombi hayo ni Septemba 16, 2012. Upatapo tangazo hili umuarifu na mwenzako.

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais.
STEMMUCO.

No comments: