Thursday, September 6, 2012

YAH: UTEUZI WA NDG. NG'HUMBUBANHU, Abel NA KUTUNUKIWA HATI YA UWAJIBIKAJI KATIKA SERIKALI KWA NDG: FRANCIS CLEMENT

Hii ni kuutaarifu Umma wa Wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara kwamba, Mhe. Rais KAMILI, John C. wa Serikali ya Wanafunzi STEMMUSO amemteua Ndg. NG'HUMBUBANHU, Abel kuwa Kiongozi mwandamizi Ofisi ya Rais, kwa ajili ya kushughulikia Masuala ya udahili wa wanafunzi hapa Chuoni. Pia katika Shughuli zake za leo Mhe.Rais amemtunuku Ndg. Clement Francis hati ya Uwajibikaji katika Serikali, pamoja na kumteua rarsmi kama Msimamizi Mwandamizi wa Ustawi wa Wanafunzi na Chuo, katika Serikali ya Wanafunzi - STEMMUSO. Pamoja na hayo Mhe.Clement ataendelea kuwa Naibu Waziri wa Habari na Masuala ya Chuo huku akifanya kazi ya Usimamizi Mwandamizi katika ofisi ya Waziri Mkuu - STEMMUSO.
Mwisho Mhe.Rais amewapongeza viongozi hawa na kuwatakia kila kheri katika utekelezaji wa majukumu yao.

"Aluta Continua" Tuongeze jitihada katika kulijenga jiji la Mungu!

SALLA, Donati P.
Makamu wa Rais
CHUO KIKUU CHA STELLA MARIS MTWARA.




No comments: