Wednesday, September 5, 2012

YAH: TANZIA YA KIFO CHA DEZDER DENICE

Uongozi wa Serikali ya Wanafunzi STEMMUSO unasikitika kuwataarifu juu ya kifo cha mwanafunzi mwenzetu aliyekuwa mwaka wa pili na kutaraji kuingia mwaka wa tatu 2012/2013 ambaye Jina lake ni DEZDER, Denice au kwa jina maarufu "Kaboy" kwamba amefariki usiku wa kuamkia Jumatatu tarehe 03 September 2012. Marehemu amezikwa kijijini kwao Rubya, Mkoani Kagera katika siku ya Jumanne tarehe 04 September 2012. Kwa upande wa Chuo, Chuo Kiliwakilishwa na Padre kutoka SAUT Main Campus na kwa upande wa serikali ya Wanafunzi, Tuliongozwa na Mhe: Deusdedith Mathius - Naibu Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi STEMMUSO. Chuo kilitoa rambirambi ya fedha taslimu kwenye familia ya marehemu na pia  baadhi ya wanafunzi wenzetu wa STEMMUCO waishio mkoani Kagera walihudhuria maziko hayo.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa! Jina la Bwana libarikiwe na Mungu ailaze roho ya marehemu pahala pema peponi Amen.

SALLA, Donati P.
Makamu wa  Rais
STELLA MARIS MTWARA UNIVERSITY COLLEGE.

No comments: