Sunday, September 2, 2012

YAH: MAJINA YA WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA STEMMUCO

Hii ni kuutaarifu Umma wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba, Majina ya watu waliochaguliwa kujinga na Chuo Kikuu Cha Stella Maris Mtwara katika programu mbalimbali yametangazwa jana rasmi na Afisa Udahili wa Chuo kupitia wavuti yetu ya www.stemmuco.ac.tz. Pia fomu za kujiunga na Chuo (Joining Instructions) zinapatikana katika wavuti hiyo ya www.stemmuco.ac.tz ikiwa ni pamoja na mchanganuo wa malipo ya ada. Kama wewe ni mmoja kati ya waliochaguliwa kujiunga na STEMMUCO, unapaswa kupakua (download) fomu inayokuhusu na kuijaza kwa umakini kisha kuja nayo hapa chuoni. Majina ya Wanafunzi waliochaguliwa katika Chuo Chetu ni wote kuanzia wale wa MBA (Master of Business Administration), Shahada ya Kwanza (Degree programmes), na Cheti katika fani mbalimbali.

SALLA, Donati P.
MAKAMU WA RAIS
STELLA MARIS MTWARA UNIVERSITY COLLEGE
 

No comments: