YALIYOJILI KATIKA KIKAO CHA SERIKALI
YA WANACHUO NA MKUU WA CHUO TOKA -2012 PIA MH. RAIS NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI
TAREHE 12 OCTOBER 2013.
[
MMKKKFHHD
MKUU WA CHUO;
M
|
Kuu wa chuo Rev Dr. Longino alimpongeza
Mh.Rais na Baraza lake la mawaziri kwa kuwa imara na amewaomba kuendeleza ushirikiano uliopo,
kwakua serikali ya wanafunzi ni daraja kubwa na kiungo muhimu kati ya wanachuo na uongozi
wa chuo.Mkuu wa chuo pia alitoa maelekezo kuwa kila somo linatakiwa kuwa
angalau na masaa 45 hadi 48 kwa semista.
Pia Alieleza sababu mbalimbali zinazosababisha mwanachuo kushindwa kumaliza
chuo kwa wakati ambazo ni ,pombe,matatizo yakifamilia,kushindwa kulipa ada na
kutokukamilisha kwa wakati Research
hivyo akawasihi wanafunzi wa mwaka wa tatu kua makini katika mambo hayo.Vilevile
akizungumza katika kikao hicho aliahidi huduma ya maji na umeme kuwa ya uhakika na pia alisisitiza wanachuo walipe ada kwa wakati.-Aliahidi kuwa
atahakikisha wanachuo wa mwaka wa tatu
wanamaliza chuo na kuhakikisha kua hakuna anayeshindwa kumaliza na anapanga kukutana
nao kujadili mustakabali wa Research..Alisisitiza kufanyia kazi hoja iliyozua mjadala
mkubwa katika kikao hicho iliyochukua zaidi ya nusu saa kuhusu PENALT katika ulipiaji
wa ada iwapo mwanachuo atachelewa kulipa
baada ya wiki mbili chuo kufunguliwa.
RAIS NA BARAZA LA MAWAZIRI.
M
|
heshimiwa Rais wa serikali ya wanachuo akiongea na baraza la mawaziri katika kikao
hicho alitoa taarifa fupi kwa baraza kuhusu kikao alichohudhuria cha SENATE na
SU-SAUT kilichofanyika Mwanza. Alitoa taarifa kwa mawaziri juu ya michuano ya SU-SAUT
kufanyika Songea mwaka huu kuanzia tarehe 28 Desemba 2013 hadi 02 January 2014
na alitoa taarifa ya walichaguliwa katika
uongozi wa SUSAUT alipohudhuria kikao huko
Mwanza.Mh Rais alieleza kua M/kiti ni Ndg
Sabatho Jivitius kutoka-SAUT-Songea Centre , makamu m/kiti ni Flora A. Yohanna kutoka RUCO-Iringa,Katibu
ni Ndg Luhanya S Luhigo kutoka SFUCHAS-Ifakara,katibu
msaidizi ni Ndg Isaya Kitundu kutoka SAUT-Mwanza na Mhasibu ni Ndg.Gaudin
Gratian kutoka MWUCE-Moshi.
Mh Rais pia alisisitiza FAINI itaanza kutekelezwa mara moja kwa yeyote atakae bainika kujihusisha
na kutoa viti vya mbao (vinavyotumika kwenye lecture rooms) nje na kuegesha
gari,pikipiki na baiskeli sehemu isiyo husika.Pia alitoa ufafanuzi juu ya kufanyika
kwa sherehe ya welcome 1st
year 2013/2014 hivi karibuni, pia kuhusu sherehe ya mahafali ya pili ya chuo itakuwa
tarehe 06 December 2013.Mh. Rais alimalizia
kwa kutaja mabadiliko aliyoyafanya katika baraza lake la mawaziri na makatibu wa
wizara mbalimbali katika kuleta ufanisi wa utekelezaji wa majukumu katika serikali ya wanachuo.Majina
ya mabadiliko hayo yametolewa katika tangazo la serikali”PUBLIC NOTICE”
Waziri wa elimu
alitolea ufafanuzi juu ya kutowekwa mapema kwa matokeo katika mtandao kuwa kulitokana
na kujumuishwa kwa majina ya wale ambao hawakumaliza
ada zao na waliokua na Incomplete final (IF) hivyo uchambuzi ulikuwa mgumu.
Waziri wa sheria
alitoa ufafanuzi juu ya mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ya STEMMUCSO
ambapo ameahidi kuanzia tarehe 14 october 2013 wanasheria wataanza kupitia katiba
ya zamani na mapema mwaka huu wa masomo 2013/2014 itakamilika.
MICHEZO:
W
|
aziri wa michezo katika taarifa yake kwa Mh.
Rais na Baraza la mawaziri alianza kwa kutoa taarifa ya ligi maarufu ya BIGSCORE,
na akatoa maana yake kuwa ni:
BI-Bishop,G-Gabriel,
S-Sport, CO-competition for R-Recreation E-Ethics mbapo mdhamini wake ni Rev
.Dr. Msafiri, waziri alieleza kuwa ligi itakuwa
na ushindani wa hali ya juu sana kwakuzingatia
kila darasa wanataka kuwa mabingwa, hali ya maandalizi ni nzuri na ratiba
imeshatoka na inapatikana katika ubao wa matangazo.Kuelekea kwenye ufunguzi
mechi mbalimbali za kirafiki zilifanyika.Siku jumapili trh 13 oct’2013 uwanja wa
jeshi kulikua na mechi kati ya mwaka wa pili na wakwanza na matokeo yalikua kwa
mwaka wa pili kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya mwaka wa kwan`Matokeo mengine kuelekea BIGSCORE ni ya
mechi kati ya 2nd yr B VS 3rd yr A ambapo timu zote
zilifungana goli 1-1 hivyo kutokua na mbabe katika mechi hiyo . 2nd
yr A score 3 Vs 2nd yr B
score 5 uwanja wa jeshini, trh 19 oct’2013.
Waziri wamichezo alitoa taarifa ya kuanza kwa mashindano ya BIGSCORE trh 26
oct’2013 na mechi za ufunguzi zitafanyika katika viwanja vya TTC.
TETESI ZA NANI ATAIBUKA BINGWA KATIKA MASHINDANO YA BIGSCORE
2013
W
|
adau na wachambuzi wa mpira hapa chuoni
wanajaribu kuipanafasi timu ya 2ndyrB kutokana na kufanya vizuri katika
mechi zake kuelekea michuano,pia 2ndyr wamekuwa wamoja kwa kila jambo
na wanatekeleza kwa wakati.Mh
waziri wa chuo,ndg.Egno alinukuliwa na mwandishi wa habari wa radio Pride fm ‘’tuna
timu nzuri,yenye wachezaji wanao jua nini
wanakifanya wawapo uwanjani na nini kiu ya mashabiki wao”, hofu yangu nikuwa
yawezekana fainali ya Mwaka huu wakakutana wanandugu’’.Timu upande wa mpira wa pete
huenda mwaka watatu (wazee wa chuo) wakanyakuwa ubingwa, kwani wanaonekana kujipanga vilivyo baadaya kuona nafasi ni finyu
katika mpira wamiguu.Kwa upande wa uvutaji kamba, volleyball na mchezo wa kukimbiza
kuku iwapo itahusika wanapewa nafasi 1styr , pia 2ndyr huenda
wakafanya vizuri katika basketball.
IMEANDALIWA NA WIZARA YA HABARI-STEMMUCSO
Kwa taarifa yoyote,tukio lolote na
maoni usisite kututumia ujumbe kwa namba na e-mail zifuatazo na taarifa yako itafanyiwa
kazi au itafikishwa mahali husika.
NO;0752068582,0715307751,0786447013,0752179863,,presidency.stemmuso@gmail.com godfreynassoro@ymail.com au danstanmahiza@gmail.com, kyalyendaguido@yahoo.com
No comments:
Post a Comment