Saturday, February 23, 2013

YAH: KUTEULIWA KWA PADRE TITUS MDOE (DPAF -STEMMUCO)

Kwa furaha kubwa na isiyo na kifani ninapenda kuchukua nafasi hii kuutaarifu umma wa wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Stella Maris Mtwara kwamba, Mheshimiwa Baba Padre Titus Joseph Mdoe wa Jimbo Katoliki la Tanga -Tanzania, ambaye alikuwa ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Kishiriki Cha Stella Maris Mtwara akishughulikia masuala ya Fedha, Utawala, na Mipango, ameteuliwa na Baba Mtakatifu Benedict XVI kuwa Mhashamu Baba Askofu Msaidizi wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam!
Utaratibu wa Kumuaga Baba Askofu Mdoe unaendelea kupangwa na Utawala wa Chuo, na Umma utafahamishwa kuhusu taratibu zote zitakazoendelea hapo baade.

Wenu katika ujenzi wa STEMMUCO

Ndg. KAMILI, John C.
Rais - Serikali ya Wanafunzi STEMMUCO.

No comments: