Sunday, October 27, 2013

STEMMUSO WEEKLY JOURNAL

YALIYOJILI KATIKA KIKAO CHA SERIKALI YA WANACHUO NA MKUU WA CHUO TOKA -2012 PIA MH. RAIS NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI TAREHE 12 OCTOBER 2013.

[
MMKKKFHHD

MKUU WA CHUO;

M
Kuu wa chuo Rev Dr. Longino alimpongeza Mh.Rais na Baraza lake la mawaziri kwa kuwa imara  na amewaomba kuendeleza ushirikiano uliopo, kwakua  serikali ya  wanafunzi ni daraja  kubwa na kiungo muhimu kati ya wanachuo na uongozi wa chuo.Mkuu wa chuo pia alitoa maelekezo kuwa kila somo linatakiwa kuwa angalau  na masaa 45 hadi 48 kwa semista. Pia Alieleza sababu mbalimbali zinazosababisha mwanachuo kushindwa kumaliza chuo kwa wakati ambazo ni ,pombe,matatizo yakifamilia,kushindwa kulipa ada na kutokukamilisha kwa wakati Research  hivyo akawasihi wanafunzi wa mwaka wa tatu kua makini katika mambo hayo.Vilevile akizungumza katika kikao hicho aliahidi huduma ya maji na umeme  kuwa ya uhakika na pia  alisisitiza wanachuo walipe  ada kwa wakati.-Aliahidi kuwa atahakikisha  wanachuo wa mwaka wa tatu wanamaliza chuo na kuhakikisha kua hakuna anayeshindwa kumaliza na anapanga kukutana nao kujadili mustakabali wa Research..Alisisitiza kufanyia kazi hoja iliyozua mjadala mkubwa katika kikao hicho iliyochukua zaidi ya nusu saa kuhusu PENALT katika ulipiaji wa ada iwapo mwanachuo atachelewa  kulipa baada ya wiki mbili chuo kufunguliwa.

RAIS NA BARAZA LA MAWAZIRI.

M
heshimiwa Rais wa serikali ya wanachuo  akiongea na baraza la mawaziri katika kikao hicho alitoa taarifa fupi kwa  baraza  kuhusu kikao alichohudhuria cha SENATE na SU-SAUT kilichofanyika Mwanza. Alitoa taarifa kwa mawaziri juu ya michuano ya SU-SAUT kufanyika Songea mwaka huu kuanzia tarehe 28 Desemba 2013 hadi 02 January 2014 na alitoa  taarifa ya walichaguliwa katika uongozi wa  SUSAUT alipohudhuria kikao huko Mwanza.Mh Rais alieleza kua M/kiti ni Ndg Sabatho Jivitius kutoka-SAUT-Songea Centre , makamu m/kiti ni Flora A. Yohanna kutoka RUCO-Iringa,Katibu ni Ndg Luhanya S Luhigo kutoka SFUCHAS-Ifakara,katibu msaidizi ni Ndg Isaya Kitundu kutoka SAUT-Mwanza na Mhasibu  ni Ndg.Gaudin Gratian kutoka MWUCE-Moshi.
Mh Rais pia alisisitiza FAINI itaanza kutekelezwa  mara moja kwa yeyote atakae bainika kujihusisha na kutoa viti vya mbao (vinavyotumika kwenye lecture rooms) nje na kuegesha gari,pikipiki na baiskeli sehemu isiyo husika.Pia alitoa ufafanuzi juu ya kufanyika kwa sherehe ya welcome 1st year 2013/2014 hivi karibuni, pia kuhusu sherehe ya mahafali ya pili ya  chuo  itakuwa tarehe 06 December 2013.Mh. Rais alimalizia kwa kutaja mabadiliko aliyoyafanya katika baraza lake la mawaziri na makatibu wa wizara mbalimbali katika kuleta ufanisi wa utekelezaji wa  majukumu katika serikali ya wanachuo.Majina ya mabadiliko hayo yametolewa katika tangazo la serikali”PUBLIC NOTICE”

Waziri wa elimu alitolea ufafanuzi juu ya kutowekwa mapema kwa matokeo katika mtandao kuwa kulitokana na  kujumuishwa kwa majina ya wale ambao hawakumaliza ada zao na waliokua na Incomplete final (IF) hivyo uchambuzi ulikuwa mgumu.
Waziri wa sheria alitoa ufafanuzi juu ya mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya ya STEMMUCSO ambapo ameahidi kuanzia tarehe 14 october 2013 wanasheria wataanza kupitia katiba ya zamani na mapema mwaka huu wa masomo 2013/2014 itakamilika.

MICHEZO:

W
aziri wa michezo katika taarifa yake kwa Mh. Rais na Baraza la mawaziri alianza kwa kutoa taarifa ya ligi maarufu ya BIGSCORE, na akatoa maana yake kuwa ni:
BI-Bishop,G-Gabriel, S-Sport, CO-competition for R-Recreation E-Ethics mbapo mdhamini wake ni Rev .Dr. Msafiri, waziri  alieleza kuwa ligi itakuwa na ushindani wa  hali ya juu sana kwakuzingatia kila darasa wanataka kuwa mabingwa, hali ya maandalizi ni nzuri na ratiba imeshatoka na inapatikana katika ubao wa matangazo.Kuelekea kwenye ufunguzi mechi mbalimbali za kirafiki zilifanyika.Siku jumapili trh 13 oct’2013 uwanja wa jeshi kulikua na mechi kati ya mwaka wa pili na wakwanza na matokeo yalikua kwa mwaka wa pili kuibuka na ushindi wa magoli 2-0 dhidi ya mwaka wa kwan`Matokeo mengine kuelekea BIGSCORE ni ya mechi kati ya  2nd yr B  VS 3rd yr A ambapo timu zote zilifungana goli 1-1 hivyo kutokua na mbabe katika mechi hiyo . 2nd yr A  score 3 Vs 2nd yr B score 5 uwanja wa jeshini, trh 19 oct’2013.
Waziri wamichezo alitoa taarifa ya  kuanza kwa mashindano ya BIGSCORE trh 26 oct’2013 na mechi za ufunguzi zitafanyika katika viwanja vya TTC.

TETESI ZA NANI ATAIBUKA BINGWA KATIKA MASHINDANO YA BIGSCORE 2013
W
adau na wachambuzi wa mpira hapa chuoni wanajaribu kuipanafasi timu ya 2ndyrB kutokana na kufanya vizuri katika mechi zake kuelekea michuano,pia 2ndyr wamekuwa wamoja kwa kila jambo na  wanatekeleza  kwa  wakati.Mh waziri wa chuo,ndg.Egno alinukuliwa na mwandishi wa habari wa radio Pride fm ‘’tuna timu nzuri,yenye wachezaji wanao jua nini  wanakifanya wawapo uwanjani na nini kiu ya mashabiki wao”, hofu yangu nikuwa yawezekana fainali ya Mwaka huu wakakutana wanandugu’’.Timu upande wa mpira wa pete huenda mwaka watatu (wazee wa chuo) wakanyakuwa ubingwa, kwani wanaonekana  kujipanga vilivyo baadaya kuona nafasi ni finyu katika mpira wamiguu.Kwa upande wa uvutaji kamba, volleyball na mchezo wa kukimbiza kuku iwapo itahusika wanapewa nafasi 1styr , pia 2ndyr huenda wakafanya vizuri katika  basketball.
IMEANDALIWA NA WIZARA YA HABARI-STEMMUCSO
Kwa taarifa yoyote,tukio lolote na maoni usisite kututumia ujumbe kwa namba na e-mail zifuatazo na taarifa yako itafanyiwa kazi au itafikishwa mahali husika.
NO;0752068582,0715307751,0786447013,0752179863,,presidency.stemmuso@gmail.com godfreynassoro@ymail.com au danstanmahiza@gmail.com, kyalyendaguido@yahoo.com


No comments: