YAH: MALIPO YA FEDHA ZA MAZOEZI KWA VITENDO, TAREHE YA KUFANYA
MITIHANI YA KUJAZILIA (SUPPLEMENTARY & SPECIAL EXAMINATIONS),
MALIPO YA FEDHA ZA UTAFITI KWA MWAKA WA TATU WALIOMALIZA
MASOMO YAO KATIKA MWAKA WA MASOMO 2011/2012, PAMOJA NA
TARATIBU ZA MAOMBI YA KOZI NA PROGRAMU MBALIMBALI KATIKA
CHUO CHETU CHA STELLA MARIS MTWARA.
Baada ya Kupokea simu na meseji mbalimbali zinazotaka ufafanuzi juu ya masuala tajwa hapo juu, kwa niaba ya Wizara ya Mikopo, Wizara ya Habari na Masuala ya Chuo, pamoja na Wizara ya Elimu, ninatoa taarifa rasmi ya masuala tajwa hapo juu kama ifuatavyo;
(1) MALIPO YA FEDHA ZA MAZOEZI KWA VITENDO.
Mheshimiwa Rais aliniagiza mnamo tarehe 16/07/2012 kufika Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu ili Serikali ya STEMMUSO, kwa niaba ya wanafunzi, iweze kupata muafaka au hatma ya malipo ya fedha za mazoezi kwa vitendo zinazofahamika kama "Boom la field" Nilikwenda tarehe 17/07/2012 kuhakiki taarifa hizo. Baada ya kufika bodi nilikuta nyaraka za ulipwaji wa fedha, pamoja na hundi ya fedha iliyokuwa imekwisha andikwa kwa ajili ya malipo ya wanafunzi wa STEMMUCO ambapo hundi hiyo pamoja na oradha ya majina ya walipwaji wa fedha hizo ilikuwa imekwisha andaliwa na Waziri wa Mikopo wa STEMMUSO kwa kushirikiana na Mwadili/Mshauri wa Wanafunzi. Niliwauliza Bodi ya Mikopo Kulikoni? Mbona kuna makaratasi lakini hakuna fedha?Bodi ya Mikopo hawakuwa na majibu yanayoeleweka ila walisema kuwa kuanzia tarehe 17/07/2012 hadi Katikati ya Mwezi wa Augusti Ndani ya kipindi hicho katika muda wowote ule Fedha za field zitaingizwa kwenye akaunti zetu. Jambo lililoonyesha wazi kabisa kwamba Bodi ya Mikopo kwa sasa hawana fedha. Hivyo basi naomba nichukue nafasi hii kuomba wanafunzi na kuwasihi kwa dhati kwamba tuwe watu wenye subira na wavumilivu katika kipindi chote hiki ambacho ni kigumu. Serikali yenu mliyoipa dhamana itahakikisha kwamba inashughulikia suala hili kwa haraka, na kwa umakini mkubwa katika muda mwafaka.
(2) TAREHE YA KUFANYA MITIHANI MAALUM NA ILE YA KUJAZILIA (Supplementary &Special Examinations)
Tarehe iliyokuwa imetangazwa awali ni tarehe 03/09/2012 - 08/09/2012. Mpaka sasa hakuna taarifa zozote za kubadilika kwa tarehe hizo ila baada ya kutangazwa kwa matokeo ya Mitahani ya semista ya pili Mnamo mwezi August, tutatoa taarifa mpya juu ya kubakia kwa tarehe tajwa kwa ajili ya ufanyaji wa mitihani hiyo, au mabadiliko ya tarehe nyingine kwa ajili ya kufanya mitahani husika.
(3) FEDHA ZA MALIPO YA UTAFITI KWA AJILI YA MWAKA WA TATU WALIOMALIZA.
Fedha hizo zipo kwa kuwa ni moja kati ya masuala niliyoyashughulikia nilipokwenda bodi ya Mikopo ila zitatoka wakati wa malipo ya fedha za mazoezi ya Vitendo kwa mwaka wa kwanza na wa pili. Kwa maelezo zaidi soma tangazo namba moja hapo juu.
(4) MAOMBI YA KUSOMA KOZI MBALIMBALI HAPA CHUONI.
Maelekezo yote ya uombaji wa kozi na programu mbalimbali hapa chuoni pamoja na taratibu na sifa za uombaji, pamoja na makataa (Deadline) ya uombaji wa kozi na programu zote yanapatikana katika tovuti ya chuo ambayo ni Http://www.stemmuco.ac.tz Hivyo basi serikali ya STEMMUSO inawashauri wadau wake kufungua wavuti ya chuo ili kupata taarifa hizo. Pia wanafunzi waliomaliza mwaka wa tatu mnamo mwaka 2011/2012 wanaruhusiwa kuomba programu ya MBA (Master of Business Administration) ilimradi tu wawe na sifa stahiki.
SALLA, Donati P.
MAKAMU WA RAIS
STEMMUSO